Kwa mujibu wa Idara ya Kimataifa ya Shirika la Habari la Hawza, makumi ya walimu na wanafunzi wa Hawza ya Najaf wamekusanyika kupinga kusitishwa safari za ndege za Iran, na wameitaka Serikali ya Iraq ifute uamuzi huo mara moja.
Inafaa kutajwa kwamba hivi karibuni Marekani imeweka vikwazo vipya dhidi ya taasisi kadhaa zinazohusiana na sekta ya usafiri wa anga ya Iran. Marekani pia imeziwekea vikwazo karibu kampuni zote za ndege za Iran.
Wizara ya Hazina ya Marekani imetishia kuiwekea vikwazo kampuni yoyote au uwanja wowote wa ndege duniani ambao utatoa huduma kwa ndege za Iran.
Maoni yako